Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, kundi la wanazuoni na maulama wa Kishia wa Georgia, katika tamko lao, walifanya upya ahadi yao ya utii kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kulaani vikali kauli za kiburi za Donald Trump.
Maandishi ya tamko ni kama ifuatavyo:
Sisi, kundi la masheikh wa Kishia wa Georgia, tunalaani kwa uthabiti vitisho vya kigaidi, njama za mauaji na vitisho vya kumuua Kiongozi Mkuu wa Dini na Marji' mkubwa wa Kiislamu, Mtukufu Ayatollah Khamenei, vinavyofanywa na nguvu za uovu na za kibeberu za dunia. Tunakemea waziwazi nia hizi za kihalifu na kutangaza uungaji mkono wetu kamili, thabiti na usiotikisika kwa Kiongozi Mkuu wa Dini.
Vitisho vya aina hii havimlengi mtu mmoja tu, bali ni shambulio lililopangwa kwa makusudi na lenye hatari kubwa dhidi ya heshima ya Umma wa Kiislamu, roho ya mapambano, maadili ya kimungu na sauti ya kudai haki ya mataifa yaliyodhulumiwa.
Leo hii, Mtukugu Ayatollah Khamenei katika ulimwengu wa Kiislamu ni nembo ya uadilifu, uhuru, njia ya Qur’ani na Ahlul-Bayt (amani iwe juu yao), pamoja na utamaduni wa kusimama dhidi ya dhuluma. Misimamo yake iliyo wazi, ya kimsingi na ya kishujaa katika kukabiliana na sera za nguvu za kibeberu na wavamizi—hasa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel—na msimamo wake thabiti katika kuwatetea watu waliodhulumiwa wa Palestina na Waislamu wa Ghaza, ameweka wazi kabisa mpaka kati ya haki na batili.
Tunaamini kwamba vitisho hivi ni kukiri wazi kwa kushindwa kisiasa na kiroho kwa nguvu za kidhalimu, na ni dalili ya kushindwa kwao mbele ya muhimili wa muqawama (Jabhatu al-Muqawama).
Historia imeonesha kwamba viongozi wa Mwenyezi Mungu hawawezi kutishwa kwa lugha ya vitisho, vurugu na ugaidi. Ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli: “Madhalimu hupanga hila, lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mpangaji bora zaidi.” Kwa msingi huo, tunawaomba Waislamu wote, wanazuoni, masheikh na watu wote huru, katika kipindi hiki nyeti na cha kihistoria, wasikae kimya, bali waoneshe umoja, mshikamano na msimamo thabiti kwa ajili ya maslahi ya juu ya Umma wa Kiislamu.
Sisi, masheikh wa Georgia, tunatangaza kwamba kusimama pamoja na Kiongozi Mkuu wa Dini si msimamo wa kisiasa tu, bali ni wajibu wa kidini, kimaadili na wa dhamiri. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amlinde Mtukufu Ayatollah Khamenei chini ya hifadhi Yake ya kimungu, aujalie Umma wa Kiislamu umoja na uelewa wa kina, avigeuze vilio vya waliodhulumiwa kuwa adhabu juu ya madhalimu, na aufikishe mhimili wa Haki kwenye ushindi wa mwisho.

Maoni yako